Biko Ad
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ushauri wa Evra kwa Ronaldo kuhusu hatma yake ya soka Real Madrid au Juventus

on

Beki wa zamani wa club ya Man United na Juventus Patrice Evra amekuwa mmoja kati ya wachezaji au wadau wa soka ambao wameamua kulizungumzia suala la tetesi za Cristiano Ronaldo kuihama Real Madrid na kudaiwa kujiunga na Juventus ya Italia.

Evra ambaye ni miongoni mwa watu wanaofuatilia kwa karibu tetesi za usajili wa Ronaldo kujiunga na Juventus, ameamua kumshauri mchezaji mwenzake huyo wa zamani ambaye wamewahi kucheza wote kwa pamoja katika club ya Man United miaka kadhaa iliyopita.

“Sijapata nafasi ya kuzungumza na Cristiano Ronaldo kuhusiana na ishu hii lakini kama anataka kucheza soka hadi mwaka 2050 anatakiwa aende Juventus maana hakuna timu nyingine ambayo anaweza kujiunga nayo, mimi nawashukuru Juve maana hata baada ya Man United walinipa nafasi ya kucheza na  kushinda mataji”>>>Evra

Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments