World Sales Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

AUDIO: Mtoto azungumzia kifo cha Mzee Samwel Sitta

on

Leo asubuhi November 7 2016 watanzania wameamka na habari za kusikitisha baada ya taarifa za kifo cha Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Samwel Sitta.

Taarifa zinasema Mzee Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.

Benjamin Sitta ni mtoto wa Marehemu Samwel Sitta hapa amezungumza kuhusu kifo cha baba yake Mzee Sitta……>>>‘Mzee alikuwa anasumbuliwa na saratani ya tezi dume ambayo imekwenda kuathiri viungo vingine, siku zote ambazo alikuwa amekwenda nje kujaribu kupambana nayo lakini kwa bahati mbaya ilienea sana na kuanza kuathiri viungo vingine mpaka miguu’

INTERVIEW: Haya hapa chini ni mahojiano ya mwisho ya Mzee Samwel Sitta na millardayo.com na AyoTV na alikua akikanusha taarifa zilizoandikwa gazetini kwamba amehamishwa kwenye nyumba ya serikali aliyokua akiishi.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement