Top Stories

Umoja wa Mataifa kuingia mkataba na Serikali kupitia Maafisa habari

on

Leo March 13, 2018 stori nayokusogezea ni kutoka mkoani Arusha ambapo Shirika la Mpango la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP umeonyesha nia  ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia chama cha maafisa habari na mawasiliano Tanzania(TAGCO) .

Katika ushirikiano huo sekta ya habari itatoa fursa kwa wanahabari kutembelea na kuitangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.

Mwenyekiti wa TAGCO, Pascal Shelutete amesema kusainiwa kwa mkataba wa mashirikiano hayo kutatoa fursa ya malengo yaliyopo baina ya serikali  ya Tanzania na umoja wa mataifa  

Nae Mkurugenzi wa idara ya habari, maelezo ambaye pia ni msemaji mkuu wa serikali, Hassan Abbas amesema mkataba huo utawawezesha maafisa habar kutekeleza kwa haraka malengo 17 ya dunia ya Milenia.

WATUHUMIWA 61 WA UGAIDI ARUSHA MAHAKAMANI

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments