Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Wananchi walivyokuwa wakitamani RC Makonda ‘amtumbue’ DMO

on

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati akiendelea na ziara yake jijini Dar es salaam alifika kata ya Pemba Mnazi Kigamboni na kukutana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza kero zao mbalimbali. Kubwa lililoibuka ni huduma inayotolewa na kituo cha afya cha eneo hilo.

RC Makonda alimuita mbele Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Kigamboni kujibu kwa nini huduma ya afya mahali hapo imekuwa si ya kuridhisha, Kaimu Mganga mkuu wa wilaya hiyo alijibu na kujitetea kuwa muda aliokaa katika ofisi hiyo ni mwezi mmoja na nusu hivyo baadhi ya changamoto hazifahamu hivyo RC Makonda alitoa agizo kuwa November 21 2016 apate majibu ya hatua gani zimechukuliwa kutatua kero za eneo hilo.

Unaweza kuangalia video hii hapa chini kujionea Wananchi walivyokuwa wakitamani DMO atumbuliwe

VIDEO: Eneo ambalo litajengwa Dampo la Kisasa Kigamboni 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement