Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Maneno ya Jurgen Klopp baada ya picha za Rooney kunaswa kalewa

on

Stori ya picha za nahodha wa timu ya taifa ya England na klabu ya Man United Wayne Rooney kutolewa akiwa amelewa na gazeti la The Sun zinazidi kugonga vichwa vya habari, tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Mourinho pekee ndio atazungumzia ishu hiyo.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa ni mmoja kati ya watu ambao hawakufurahishwa na tabia hiyo ya Rooney kiasi cha kueleza shujaa unakunywa pombe na kulewa kama shetani, Rooney alinaswa na The Sun akiwa kalewa katika harusi huku akionekana na mavazi yake ya timu ya taifa.

rooney-drunk

“Siku hizi kwa vizazi hivi vya wachezaji professional sio tu England hatujawahi kusikia wala kuona mkongwe yoyote duniani akilewa kama shetani na wanavuta kama machizi bado wakaendelea kuwa wachezaji wazuri sijui, mimi sijawahi kuona”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement