Habari za Mastaa

Jay Z & Beyonce watumia wimbo wa Kiswahili katika Tamasha la Global Citizen

on

Cheki Jay Z na Beyonce walivyoingia na wimbo wa ‘Malaika’ wa Marehemu Miriam Makeba ambapo wimbo huo ni toleo la mwaka 1972 uliopatikana ndani ya Album Miriam Makeba Live In Africa wimbo huo ulitungwa na kuimbwa na Mtanzania Adam Salim mwaka 1945.

Beyonce na Jay Z wakiwa miongoni mwa wasanii wakubwa waliotoa burudani katika tamasha la Global Citizen Festival lililofanyika December 2,2018 katika uwanja wa FNB Johannesburg, Afrika Kusini katika maadhimisho ya miaka 100 ya Hayati Nelson Mandela waliingia pia na wimbo wa Tekno ‘Pana’.

Tamasha hilo liliudhuriwa na wasanii wakali wakiwemo Cassper Nyovest, Wiz Kid, Tiwa Savage, Pharrel Williams, Usher,  Sho Madjozi, Chris Martin, Eddie Vedder, D’Banj, Femi Kuti.

EXCLUSIVE: CHALII YA CHUGA BENEFICIAL KAFUNGUKA “NI HUYO MIMI”

Soma na hizi

Tupia Comments