AyoTV

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

on

Game ya Simba na Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam siku ya Jumapili ya September 30 2018 ilimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kutoka sare tasa ya 0-0.

Baada ya mchezo wengi waliikosoa Yanga kuwa ilizidiwa zaidi na Simba licha ya kufanikiwa kutoka sare hiyo, Simba waliutawala mchezo kwa asilimia 62 Yanga asilimia 38, hivyo baada ya game kocha mkuu wa Yanga mbele ya waandishi wa habari alieleza kwa nini Simba waliutawala mchezo.

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kuwa Simba kuutawala mchezo ilikuwa ni mpango wao wa kuiacha Simba itawale mchezo zaidi ya Yanga, hivyo wanaosema kuwa walizidiwa anakubali ndio lakini ni kutokana na game plan yao ya leo ilikuwa ni kuwaachia Simba watawale mchezo.

Mtoto raia wa New Zealand kaja Taifa kuisapoti Simba ishinde 100-0 vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments