Tangaza Hapa Ad

Magazeti

Gereza aliko mbunge Peter Lijualikali labainishwa

on

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.

Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Nipashe, yenye kichwa cha habari ‘Gereza aliko mbunge CHADEMA labainishwa’ 

Gazeti hilo limeripoti kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro kupitia chama cha Demokrasia  na maendeleo ‘CHADEMA’, Peter Lijualikali  yupo katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Jumatano iliyopita, mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimhukumu kumikia kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini mbunge huyo kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza na Gazeti la Nipashe jana kwa simu, alisema alimtembelea mbunge huyo kwenye gereza la Ukonga alikofungwa mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Unaweza kupitia hapa chini nyingine kubwa 10 kutoka kwenye magazeti ya leo

AyoTVMAGAZETI Viongozi watatu wa Chadema wafungwa, Ujenzi wa hospitali wamng’oa kigogo, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement