DSTV

Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Wema Sepetu aendelea kuwa kimya baada ya Lipstick zake kufungiwa na Serikali

on

Ni miaka mitatu imepita tokea Wema Sepetu Miss Tanzania 2006 azindue lipstick zake ziitwazo “Kiss By Wema Sepetu” na zikaingia sokoni na kufanya vizuri kwenye mauzo sehemu mbalimbali za Tanzania.

Leo November 11 2017 Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetangaza kuzifungua lipstick hizo na kueleza kwamba wamebaini kuwa hazijakidhi viwango vya matumizi kwa binadamu.

Tulizoea kuona Wema Sepetu akijibu haraka au kuzungumzia matukio yake pindi tu yakitokea kama hivi lakini kwenye hili la leo bado ameendelea kuwa kimya na kutoandika chochote kulihusu kwenye mitandao yake.

Kwenye mitandao yake leo Wema ameichunia habari ya kufungiwa na badala yake ameendelea kuipigia debe APP yake mpya ya kulipia ambayo itakua ikionyesha mambo yake mbalimbali ikiwemo movie anazoigiza pamoja na maisha yake ambapo kwenye moja ya post zake alizopost jioni ya November 11 2017 imesomeka hivi hapa chini.

Najivunia Kuwa The First Female in AFRICA to own my Very Own Application, Mnadhani naskia sifa wala… Sioni hata sifa… (LoveDove??? Download WemaApp now on Playstore… Soon itafika mpaka App Store… Inshallah

“MIMI NA WEMA SEPETU TUNAKUTANA SANA”DIAMOND PLATNUMZ

RED CARPET: “WEMA NA IDRIS WAMERUDIANA? MTU KASHIKWA MKONO MWANZO MWISHO

EXCLUSIVE: WEMA SEPETU AELEZA KWANINI ALIFUTA PICHA ZOTE INSTAGRAM….

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement