Michezo

Mwinyi Zahera atoa tamko kuhusu Beno Kakolanya kugoma

on

Golikipa wa Yanga Beno Kakolanya kwa zaidi ya wiki kadhaa sasa amekuwa hayupo kikosini kwa madai ya kugoma kujiunga na timu hiyo ili ashinikize kulipwa pesa zake za usajili ambazo amekuwa akiidai Yanga kwa muda mrefu sasa.

Kakolanya ambaye amegoma kujiunga na wachezaji wenzake kwa zaidi ya wiki sasa, kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera ameongea na Azam TV na kufunguka msimamo wake kuhusiana na mgomo wa mchezaji huyo kubwa akisema hawezi kumlazimisha mchezaji aje mazoezini.

“Mimi nasikia tu kwa watu ndio wananiambia kuwa Beno Kakolanya kagoma kusafiri na timu, sina hata habari moja kuwa Kakolanya anaondoka mimi natoka timu ya Taifa Congo naambiwa Kakolanya kagoma kusafiri na timu kama mchezaji aligoma kusafiri na timu hakunipigia simu mimi siwezi kumpigia, mchezaji kama anakataa kwenda mazoezi mimi kocha siwezi kukufuata”>>>>Mwinyi Zahera

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments