Tangaza Hapa Ad

Mix

Maamuzi ya mahakama kuu Arusha kuhusu rufaa ya kupinga kumnyima dhamana Lema

on

Leo December 2 2016 Mahakama kuu kanda ya Arusha imetupa rufaa ya kupinga maamuzi ya kumnyima dhamana iliyoamuliwa na mahakama ya hakimu mkazi dhidi ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema.

Naibu msajili wa Mahakama kuu kanda ya Arusha, Anjelo Rumisha amesema kwamba rufaa hiyo ilikuwa imekatwa nje muda uliopangwa.

Akizungumza baada ya maamuzi hayo, wakili wa Lema, John Malya amesema wameongea na mteja wao na kuwaambia wasishughulike tena na kesi hiyo hadi pale upande wa Jamhuri utakapoamua lakini wao wataendelea kukutana na jopo la mawakili ili kuja na njia mbadala

AyoTVMAGAZETI: Biashara usafiri wa ndege pasua kichwa, Wapinzani wampa JPM mambo 9 ya kuzingatia, Bonyeza play hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement