Tangaza Hapa Ad

Magazeti

Kabila linalotumia silaha ya Gobore kama sehemu ya mahari

on

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.

Moja ya habari iliyoandikwa leo January 7 2017 ni pamoja na hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Gobore latumika sehemu ya mahari’

Gazeti hilo limeripoti kuwa mila ya kutoa silaha aina ya gobore kama sehemu ya mahari kwa kabila la Wapimbwe, waishio wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imetajwa kuwa moja ya sababu za kuongezeka kuzagaa kwa silaha mkoani hapo.

Mwanaume anapomuoa msichana katika kabila hilo, hutakiwa pamoja na mambo mengine kutoa gobore, hivyo kulazimika kutafuta watu wanaotengeneza magobore hayo ili wamtengenezee ili akalipe mahari na kupata mke.

Mmoja wa wazee wa kabila la Wapimbwe, Christopher Kapama, akizungumza na Gazeti la Nipashe alisema hiyo imekuwa ni sababu zinazochangia mkoa wa Katavi kuonekana kuna bunduki nyingi za aina ya magobore zikiwa zimezagaa maeneo mbalimbali.

Alisema kwa asili, kabila la Wapimbwe ni wawindaji na miaka ya nyuma walikuwa wanadai gobore kama sehemu ya mahari ili iwasaide katika shughuli zao, lakini kutokana na sheria za wanyamapori hivi sasa uwindaji wa aina hiyo ni haramu hivyo inabidi mila hiyo ibadilike.

Unaweza kuzipitia hapa chini habari zingine kubwa za magazeti ya leo January 7 2017

AyoTVMAGAZETI: Vigingi 9 tishio kwa boss mpya TANESCO, Familia majeruhi 4,000 zaibebesha mzigo MOI 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement