Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Kero nne zilizoibuliwa na wakazi wa Keko DSM mbele ya RC Makonda

on

Leo November 21 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ameendelea na ziara yake jijini Dar es salaam ambapo leo ilikuwa ni siku ya tatu na ameanza ziara yake wilaya ya Temeke na akiwa katika ziara yake msafara wake ulisimama eneo la keko Furniture ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa samani na akasikiliza kero za wafanyabiashara wa eneo hilo.

Alipofika eneo hilo la keko waliibua kero zao ambazo RC Makonda aliita watendaji husika kujibu kero hizo, baadhi ya kero zilizoelezwa ni pamoja na kukamatwa na polisi wanapowaona wamebeba samani na kutozwa faini, Bodaboda wanaumizwa na polisi kwa kusukumwa mpaka wanaumia, Kituo cha polisi Chang’ombe askari wanapokea rushwa na kingine walichokizungumza ni kuwa kuna baadhi ya mitaa unakamatwa hata kama unasaidia wengine.

Unaweza kuangalia video hii hapa chini kuhusu kero hizo na majibu yake

VIDEO: Eneo ambalo litajengwa Dampo la Kisasa Kigamboni 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement