Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Tamko la Jeshi la polisi kwa ambao hawajahakiki silaha zao

on

Katika kipindi cha kuanzia march 22 2016 hadi June 30 2016 Serikali ilifanya zoezi la uhakiki wa silaha zote za kiraia Tanzania bara. Baada ya zoezi hilo kukamilika Makao makuu ya Jeshi la polisi wametoa tathmini ambapo imeonyesha kuwa asilimia 59.18 tu ya silaha zote zilizosajiliwa ndiyo zilihakikiwa wakati 40.82 hazijahakikiwa kwa sababu wamiliki hawakujitokeza kuzihakiki..

Leo November 18 2016 makao makuu ya jeshi la polisi kupitia kwa kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, Robert Boaz amesema kuwa kwa sababu wanatambua huenda zipo sababu za msingi kwa baadhi ya wamiliki kushindwa kujitokeza hivyo wamewataka wamiliki ambao hawajahakiki silaha zao kuhakiki silaha zao ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia November 11 hadi December 20 2016 na utakapomalizika watachukua hatua kali.

VIDEO: Polisi Makao makuu kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya kamanda Sirro 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement