Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Anna Mugwhira ACT ajibu swali la Zitto Kabwe yuko wapi?

on

Baada ya taarifa kutoka jeshi la polisi Shinyanga kuhusu kukamatwa kwa gari alilokua analitumia kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO ambae pia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto kabwe.

Ilidaiwa kwamba sababu ya gari hilo kukamatwa ni kosa la kutokuwa na vibali halali huku Polisi ikimtaka Zitto ajitokeze.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mama Anna Mugwhira ameongea na AzamTV kuhusu uwepo wa taarifa za kutoonekana kwa kiongozi wa ACT Zitto Kabwe.

‘Zitto alikuwa anatafutwa na polisi na mimi nilikuja kusikia gari limekamatwa lakini yeye aonekani, inaonekana yeye aliposhuka aliondoka na njia nyingine tofauti hakuondoka na gari lake, sisi kama chama hatukufikia mahali pa kufikiri kwamba hayupo au haonekani na taarifa zilizokuwa zinapatikana zilisema yupo Kahama, taarifa rasmi haijatolewa na yeye mwenyewe’;-Anna Mugwhira

ULIKOSA? POLISI WALICHOONGEA KUHUSU KUKAMATA GARI LA ZITTO KABWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement