Habari za Mastaa

LULU DIVA KAFUNGUKA: Ni baada ya kukutana na Jah Prayzah

on

Mwimbaji staa wa kike Lulu Diva Kutoka Bongoflevani amekutana na mwimbaji staa wa Zimbabwe EXQ ambaye yupo chini ya Label ya Military Touch inayomilikiwa na msanii wa Zimbabwe Jah Prayzah, ambapo amefanikiwa kupata collabo ya kwanza ya kimataifa na msanii huyo.

Lulu diva ameelezea jinsi alivyoipata hiyo collabo ambapo amesema kuwa …>>>”Jah Prayzah najuana nae since naenda south ku-shoot ngoma yangu ya pili ya Usimwache tokea hapo amekuwa akiona kazi zangu Chanel kubwa Kama MTV,Trace na zingine so huwa ananifatilia na kunipongeza kwa juhudi anazoziona nazifanya katika mziki wangu”

“Aliniambia anakuja Tanzania akifika tuonane alipofika alinitafuta na kuniomba nifanye collabo na msanii wake ambaye yupo chini yake akanisikilizisha nyimbo nikaiona ni nzuri na Mimi naweza fanya kitu kizuri kwa hiyo sikusita kutoa jibu nilikubali hapo hapo sababu niliona ntapata faida Kwani ntaongeza mashabiki kutoka Zimbabwe na fanbase yangu itaongezeka” – Lulu Diva

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza Full Story..

VIDEO:Show ya Rosa Ree FIESTA MWANZA 2017

Soma na hizi

Tupia Comments