Tangaza Hapa Ad

Mix

PICHA 3: Mchina afariki baada ya kukandamizwa na mtambo wa kushindilia lami Arusha

on

Ujenzi wa barabara ya kuanzia Tengeru Arusha hadi Taveta Voi ya ukubwa wa km 234.3 iliyozinduliwa March 3 mwaka huu na Rais John Magufuli, wakati ujenzi ukiendelea kumetokea ajali ambapo Raia wa china Injinia Yao Sijiu Pil amekandamizwa na mtambo wa kushindilia lami na kufariki dunia. 

Kwa mujibu wa balozi wa eneo la kwa mrefu ambaye pia ni shuhuda amesema marehemu alikuwa akisimamia zoezi la kushindilia lami kwenye barabara na mwendesha mtambo hakumuona, jambo lililopelekea  suruali yake kushikwa na nondo iliyokuwa karibu hivyo akaangukia barabarani na mtambo ukamkanyaga.

Jeshi la polisi kupitia kwa kaimu kamanda wa polisi Arusha Yusuph Ilembo amesema kwamba mtuhumiwa aliyesababisha kifo hicho kwa uzembe bado anashikiliwa na polisi na uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani.

1111

mashuhuda wa tukio

222 333

ULIKOSA VIVUTIO VINNE VINAVYOFIKIKA KIRAHISI ARUSHA ? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Tupia Comments

Advertisement