Tangaza Hapa Ad

Mix

AUDIO: Zilizonifikia kuhusu hali ya Godbless Lema baada ya kugoma kula mahabusu

on

Moja ya headline kutokea Arusha August 28 2016 ni pamoja na hii ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kudaiwa kuwa katika hali mbaya ya kiafya mara baada ya kugoma kula kwa siku mbili mfululizo akiwa mahabusu baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya kichochezi.

Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha Kalist Lazaro  amekutana na waandishi wa habari leo na kuongelea tukio hilo mara baada ya kutoka kumtembelea Lema akiwa mahabusu….>>>’Nimetoka kuangalia hali ya Lema lakini imeshindikana kumuwekea dhamana hadi sasa kwa madai bado wanaendelea na upelelezi

Lakini hali ya mbunge sio nzuri sababu tangu jana amegoma kula kwakuwa anasema amedhalilishwa hivyo ataendelea hivyo hadi atakapopelekwa mahakamani, kesi wanayomtuhumu ni  kufanya uchochezi kwa njia ya mtandao‘ –Kalist Lazaro

‘Tumefanya jitihada za kumshawishi ale lakini amegoma na hali yake ya kiafya imedhoofu, tunacholiomba Jeshi la Polisi wamuachie ili jumatatu aje kuripoti‘ –Kalist Lazaro

Hata hivyo kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amesema amepokea taarifa za Godbless Lema  lakini amesema wataendelea kumshikilia hadi hapo upelelezi utakapokamilika na watampeleka mahakamani.

Unaweza kuendelea kumsikiliza katibu wa CHADEMA hapa chini…

WALICHOKIONGEA MASHUHUDA WA TUKIO LA MAPIGANO YA POLISI NA MAJAMBAZI MKURANGA

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement