Top Stories

George Weah amezungumza kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais

on

George Weah amezungumza kwa mara ya kwanza tangu atangazwe Ijumaa kuwa mshindi wa kiti cha Urais nchini Liberia katika uchaguzi wa marudio, amesema ataunda serikali ambayo itajikita katika kuboresha maisha ya watu wa Liberia.

Weah ameahidi kuboresha maisha ya watu wa Liberia amesema ndicho kitakuwa kipaumbele chake  cha kwanza atakapoingia madarakani mwezi Januari.

Katika hatua nyingine, mchezaji huyo wa zamani wa mpira wa miguu, amesema wale wote wanaopenda kuwadanganya watu kwa njia za rushwa hawatakuwa na nafasi katika serikali yake.

Weah amesema utawala wake utajengwa katika misingi ya kitaasisi kama alivyoanzisha Rais Ellen Johnson Sirleaf na amewaita raia wa Liberia walioko nchi za nje warejee kushuhudia maisha mapya na bora.

“TUSIKAE KIMYA TUKIONA HATUTENDEWI HAKI” – HUSSEIN BASHE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

“KAKOBE ASIFANYE KANISA LAKE KICHAKA CHA KUFANYIA SIASA” -Rc. Gambo, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments