Top Stories

Jamaa anasa barabarani baada ya Lami kuyeyuka

on

Leo July 8, 2018 Mwanamume mmoja nchini Uingereza mwenye miaka 24 amewashangaza wengi baada ya kukwama kwenye lami iliyokuwa imeyeyuka katika barabara moja akielekea dukani.

Kijana huyo aliwapigia maafisa wa huduma za dharura kupitia nambari 999 baada ya mguu wake wa kushoto kukwama hadi pajani katika barabara moja ya pembeni eneo la Heaton, Newcastle.

Maafisa wa huduma za dharura walilazimika kuchimbua barabara eneo alipokuwa amekwama wakitumia nyundo ili kuutoa mguu wake.

Kijana huyo alinusurika bila jeraha kwa kuwa alikuwa amevaa buti ambazo hufika hadi magotini.

Msemaji wa zima moto amesema tukio hilo lilisababishwa na jua kali ambalo limekuwa likiwaka eneo hilo.

KIPAJI CHA AJABU: Anapiga beat kwa mdomo na kuimba, anaongea sauti tatu wakati mmoja

Soma na hizi

Tupia Comments