PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Habari za Mastaa

Cheki muonekano wa duka la Wema Sepetu

on

Miss Tanzania 2006 na muigizaji Wema Sepetu amerudi tena kwenye headlines baada ya wengi kudai kuwa anakaribia kufungua duka lake mwenyewe lenye jina la “Little sweethearts” hivi karibuni.

Tetesi hizo zimezuka baada ya Wema Sepetu kuonekana akiwa ameenda China na baadhi ya videos zikimuonyesha akiwa anarudi Tanzania huku akiwa na mizigo mingi  ambayo inasadikika ni kwaajili ya biashara.

Duka hilo linadaiwa kuwa litakuwa likiuza nguo za watoto na huku baadhi ya picha ya muonekano wa duka hilo limesambaa kwenye mitandao ya kijamii, marafiki wa karibu wa Wema Sepetu wameonekana pia kumpongeza kwa jitihada hizo kurasa zao za instagram.

Kilichomfanya Irene Uwoya na Tausi wakamatwe na Polisi Mbeya

Soma na hizi

Tupia Comments