Top Stories

Dada wa kazi aliyemuua Boss wake na kichanga akamatwa

on

Leo June 11, 2018 nakusogezea stori kumhusu Mfanyakazi wa ndani aliyemuua mwajiri wake pamoja na mtoto wake mwenye miezi mitatu huko Muhoroni, Kisumu nchini Kenya na kutokomea kusikojulikana amekamatwa Uganda na jeshi la polisi la nchi hiyo.

Jacky Auma alikamatwa katika eneo la Namayisi nchini Uganda baada ya jeshi la Polisi nchini Kenya kuwapa taarifa juu ya mtuthumiwa huyo kukimbilia katika mipaka ya nchi hio.

Jacky anatuhumiwa kutenda tukio hilo wiki iliyopita kwa kumpiga mtoto wa mwajiri wake mpaka kufa kisha akamchoma mwajiri wake na kisu mara kadhaa kabla ya kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali na kumfanya apoteze uhai wake.

Aidha Afisa Polisi wa kituo cha Busia amethibitisha kukamatwa kwa Jacky na amesema kuwa wako wanaandaa utaratibu ili mtuhumiwa huyo arudishwe nchini Kenya akafunguliwe mashitaka.

Maagizo aliyotoa Naibu Waziri Kilimo Dr. Mwanjelwa katika ziara Njombe

Soma na hizi

Tupia Comments