Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mourinho kachukua kipigo “Sasa mnanielewa kwa nini kila siku Lukaku”

on

Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 imeendelea tena leo kwa mchezo mmoja kati ya Brighton dhidi ya Man United katika uwanja wa American Express huo ukiwa  ni mchezo wa 36 wa Man United wa Ligi Kuu England msimu huu.

Mchezo huo umemalizika kwa Man United kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Brighton goli ambalo lilifungwa na Pascal Gross dakika ya 57, kutokana na Brighton kuwa nafasi ya 11 katika Ligi na Man United ya pili wengi walijua Man United itakuwa rashisi kupata matokeo.

Baada ya game hiyo kocha wa Man United Jose Mourinho ametoa kauli ya kushangaza na ikitafsiriwa kama kuilaumu safu yake ya ushambuliaji na kueleza kuwa watu wasimlaumu wasiendele kumlaumu kwa nini anampa nafasi sana Romelu Lukaku ambaye wengi wanadhani hastahili, Lukaku leo hakuwepo kutokana na kuwa na jeraha la enka alilolipata katika game dhidi ya Arsenal.

“Kila siku mnauliza kwani nini Lukaku kwa nini Lukaku nafikiri sasa mtakuwa na majibu yenu vichwani kwa nini kila siku Lukaku, wachezaji ambao wamekuwa wakichukua nafasi za wengine hawaoneshi uwezo nafikiri sasa mnanielewa kwa nini wachezaji wengine wanapata nafasi ya kucheza sana na uulizi kwa nini A, B, C, D”>>> Jose Mourinho

VIDEO: Mbwembwe za Haji Manara uwanjani baada ya ushindi wa Simba vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments