Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kocha wa zamani wa Yanga amefariki Dunia nchini Malawi

on

Tasnia ya soka leo imezipokea taarifa za kifo cha kocha wa zamani wa club ya Yanga raia wa Malawi Jack Chamangwana ambaye umauti umemfika akiwa hospitali.

Kocha Jack Chamangwana  umauti umemkuta akiwa na umri wa miaka 61 ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Queen Elizabeth Central mjini Blantyre nchini Malawi.

Pamoja na kuwa kocha wa vilabu mbalimbali Jack Chamangwana alikuwa kocha msaidizi timu ya taifa ya Malawi akiwa chini ya kocha mkuu Young Chimodzi na walifukuzwa kazi wote na chama cha soka Malawi 2015.

VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL

Soma na hizi

Tupia Comments