Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Ukweli juu ya Collabo ya Ney wa Mitego na Madee uko hapa.

on

neyMbali na kuwa wanatokea eneo moja la Manzese wamewahi kutangazwa kuhusu kuwa na uhasama kwa muda mrefu sana ambapo pia ilifikia kipindi mpaka familia zao zikawa na taarifa juu ya uhasama walionao,kulingana na wingi wa show walizokutana nazo kwa mwaka jana imekua rahisi kuweka tofauti zao pembeni.

madee-300x160Miongoni mwa vitu alivyovizungumza Madee baada ya Mic ya Millardayo.com kumtembelea ni kuhusu Collabo yake na Ney wa Mitego,Madee alianza kwa kusema>>’Hizo taarifa zipo hata sijui wewe umezipataje tulitaka ziwe chini chini kwanza kisha tuzitangaze hizo taarifa zipo zikishakua kamili tulitaka kuleta cd ikiwa tayari halafu ndiyo tuseme hii ndo ya nyimbo ya Madee na Ney’

‘Bado haijawa official na ngoma hatujajua inaitwaje na Marco chali ndio aliyetoa wazo hilo na sisi tutalisimamia tushaaka sana na Ney tukalizungumza unajua mapromota wengi wakimuita Madee basi kichwani mwake anataka awepo na Ney so tushakutana mara nyingi sana na moja wapo ya vitu tulivyowahi kuviongea ni pamoja na collabo yetu’.

Msikilize Madee hapo chini kwa kubonyeza play.

Tupia Comments

Advertisement