Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

Mtoto wa miaka mitatu akutwa amekufa juu ya dari Mwanza

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya yaliyondikwa kwenye gazeti la Mtanzania ni ripoti ya utafiti huu wenye kichwa cha habari ‘Mtoto akutwa amekufa juu ya dari 

Mtoto Rachel Revocatus (3) wa mtaa wa Nyasaka Center wilayani Ilemela aliyepotea kwa saa 48 amekutwa amekufa juu ya dari la chumba cha Ramdhani Musingi aliyepanga nyumbani kwao mtoto huyo. Habari zinasema mtoto huyo alipotea katika  mazingira ya kutatanisha wakati akicheza na watoto wenzake.

Tukio hilo lilitokea juzi  saa 4:00 asubuhi baada ya mke wa Musingi kuona damu inachuruzika kutoka juu ya dari la chumba chao.

Aliamua kupanda juu ya ndoo kuchungulia ni nini hasa kilikua kinatoa damu hiyo ndipo alipoona gauni la kitenge alilokua amevaa mtoto Rachel aliyepotea jumamosi iliyopita saa 4:00 asubuhi.

Akisimulia mkasa huo mama mzazi wa Rachel, Angelina James alisema aligundua mwanae alikua amepotea september 17 mwaka huu mchana alipomtafuta kwa ajili ya chakula cha mchana.

Mama huyo alisema aliwauliza wapangaji pamoja na watoto wenzake waliokua wakicheza nae kama walikua wamemuona.

Alisema baada ya kutofanikiwa kumuona saa 9:00 alasiri alikwenda kwa uongozi wa mtaa huo kutoa taarifa kama mtu ataonekana na mtoto asiye wake aulizwe, vilevile alitoa tangazo msikitini na kanisani juzi kuhusu kupotea kwa mtoto wake.

Mjomba wa mtoto huyo Johnson Charles, alisema juzi saa 4:00 asubuhi wakati wakiendelea na harakati za kumtafuta Rachel, Musingi alifika nyumbani kwao akawaelezea kuwa mtoto huyo alikutwa juu ya dari la chumba chao akiwa amekwisha kufariki dunia.

Charles alisema mpangaji huyo aliwaeleza kuwa Rachel alifariki dunia akiwa chumbani kwao baaada ya kunaswa na umeme na mdogo wake (jina limehifadhiwa) akaamua kumpandisha juu ya dari kwa hofu.

Unaweza kupitia habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania September 21 2016

 

 

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 21 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI 

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement