Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

UTAFITI: Nyimbo za Rihanna zatajwa kutuliza maumivu kwa watoto

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.

Moja ya taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ya October 25 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Nyimbo za Rihanna zinatuliza maumivu wakati wa upasuaji’

Gazeti hilo limeripoti utafiti unaodai kuwa kumsikilizisha mgonjwa nyimbo za mwanamziki maarufu wa muziki ‘pop’ Rihanna, kunamsaidia mgonjwa kupunguza maumivu wakati wa upasuaji pia kunamfanya aweze kupumua vizuri bila ya msaada wa hewa ya oksijeni.

Utafiti huo ulioendeshwa na wataalam wa hospitali ya watoto ya Lurie Chicago Marekani, umeonyesha kuwa watoto waliosikiliza nyimbo za Rihanna kwa dakika 30 wakati wa upasuaji hawakuhisi maumivu na walipumua vizuri.

Jambo hilo limefanywa chini ya utafiti wenye kulenga kutibu kwa njia ya sauti (audio therapy) unaoendeshwa na jopo la madaktari wanaoongozwa na Dk. Santhanam Suresh.

Akieleza suala hili katikaa taarifa ya utafiti wa Dk. Suresh alisema ‘Audio Therapy’ inapaswa kuchukuliwa na hospitali kama njia muhimu na bora ya kuondoa maumivu kwa watoto wanaofanyiwa upasuaji mkubwa.

Utafiti huo unachukuliwa kama sehemu muhimu ya mabadiliko ya upasuaji katika hospitali nyingi duniani kwa vile tiba ya upasuaji kwa sasa hufanywa bila ya mgonjwa kupewa dawa za kupoteza fahamu zake, maarufu kama nusu kaputi.

Kabla ya utafiti huo, Wataalamu wa masuala ya saikolojia walishagundua njia ya kutuliza akili za wagonjwa kwa kutumia rangi na wameielezea rangi ya pinki kama moja ya rangi zinazotuliza akili haraka kuliko rangi nyingine.

Wanasema kupaka rangi hiyo kwenye wodi au vyumba vya kulala, kunasaidia mgonjwa na mtu wa kawaida kutuliza akili yake na kutokuwa na mawazo mengi ikilinganishwa na rangi nyingine.

Unaweza kupitia ghabari nyingine kwenye magazeti ya Tanzania

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO YV OCTOBER 25 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement