Tangaza Hapa Ad

Mix

Majibu ya Hospitali juu ya kijana aliyetobolewa macho na Scorpion

on

Leo October 7, 2016 Millardayo na Ayo TV zimepata taarifa ya majibu ya madaktari juu ya uchunguzi wa Macho ya kijana Said maaarufu kama Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.

Jitihada zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona.

side-2

Majibu ya madaktari yametolewa leo na Mkuu wa Dar es salaam Paul Makonda na kuzua hali ya huzuni kwa Said na familia yake wakiwemo mama mzazi, mama mkwe na mkewe baada ya ripoti ya Madaktari kuonesha kwamba hakuna uwezekano wa aina yoyote ambao unaweza kumfanya kijana huyo akaja kuona tena.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Mkaonda amesema Serikali ya Mkoa itampa Said kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwaajili ya kuanzisha biashara itakayomsaidia yeye na familia yake, pia amesema kutakua na gari ambayo itakua ikimsaidia kwenye matibabu yake pamoja na kumsomesha kwenye shule za watu wenye ulemavu wa macho.

Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.

A photo posted by Paul Makonda (@paulmakonda) on

ULIMISS ALICHOKISEMA NAIBU SPIKA TULIA AKSON KUHUSU WATUW ENYE ULEMAVU WA MACHO

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement