PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Aliyosema Freeman Mbowe kuhusu kuokotwa kwa Mwili wa Katibu wa CHADEMA Hananasifu

on

Katibu wa kata ya Hananasifu Kinondoni (CHADEMA) amefariki kwenye mazingira yenye utata baada ya mwili wake kukutwa na jeraha la panga kichwani na sehemu nyingine ya mwili.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amelizungumzia tukio hilo na kusema Chama kinatoa taarifa za awali kuhusiana na msiba huu, hili ni jambo la ghafla hata ndugu wengine wa Marehemu bado hawajajua.

“Tunawaambia Wanachama wetu waendelee kuwa waangalifu wasitembee mmojammoja kati ya sasa mpaka siku ya Uchaguzi watembee kwa vikundi na wajiweke katika mazingira ya kujilinda wakati wote”

“Tangu taarifa hizi zimetolewa kwa jeshi la polisi na Viongozi wetu, zilitolewa sambamba na taarifa za mtu kupotea na kwamba aliyepotea alichukuliwa na Land Rover nyeupe na watu waliojifanya ni Jeshi la Polisi lakini tangu wakati huo hakuna taarifa yoyote ya jeshi la Polisi ya kiuchunguzi na hata kwenda kuukuta mwili ule Muhimbili tumeukuta sisi kwa jitihada zetu lakini polisi hawakutoa taarifa wameokota mwili Coco beach”

“Taarifa kwamba mwili umeokotwa maeneo ya Oysterbay ukiwa na majeraha ukapelekwa polisi tumekuta yamejazwa kwenye kitabu cha Muhimbili, lakini polisi tulipokwenda kutoa hizo taarifa walisema hawana taarifa za mtu yeyote kupotea wala hawajua chochote kuhusu jambo hili kumbe wao ndio wamepeleka mwili polisi”

1. Mambo haya yanaendekezwa, polisi wanayaona,polisi wanaonea watu wetu,polisi wananyanyasa watu wetu, tumelalamika mara nyingi mpaka tumefika hatua ya kususia chaguzi,tukafikiria labda wenzetu wanajifunza kwa hili lakini bado tunaona Serikali, Viongozi wa Serikali, Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watu ambao wangestahili kusimamia haki kwa pande zote, ndo hao hao wanakwenda kusababisha machafuko, malumbano, matusi, kuwagawa wananchi, kuigawa jamii hadi sasa tunaonekana kuna watu kazi yao ni kuua watu inagadhilika kukubali kuendelea kuuwawa. Chama kinatoa taarifa za awali kuhusiana na msiba huu, hilo ni jambo la gafla hata ndugu wengine wa marehemu bado hawajajua kuhusu taarifa hizi, lakini tumeona tutoe taarifa za awali kwanza, tunawaambia wanachama wetu waendelee kuwa waangalifu wasitembee mmoja mmoja kati ya sasa mpaka siku ya Uchaguzi watembee kwa vikundi na wajiweke katika mazingira ya kujilinda wakati wote. Vyombo vya dola ambavyo tungetegemea viwe ni walinzi wa raia wote bila kubagua vimeonekana kuwa na ubaguzi wa kina kwenye jambo hili. Tangu taarifa hizi zimetolewa kwa jeshi la polisi na viongozi wetu, zilitolewa sambamba na taarifa za mtu kupotea na kwamba aliyepotea alichukuliwa na land rover nyeupe na watu waliojifanya ni jeshi la polisi lakini tangu wakati huo hakuna taarifa yoyote ya jeshi la polisi ya kiuchunguzi na hata kwenda kuukuta mwili ule Muhimbili tumeukuta sisi kwa jitihada zetu lakini polisi hawakutoa taarifa wameokota mwili Coco beach. Taarifa kwamba mwili umeokotwa maeneo ya Oysterbay ukiwa na majeraha ukapelekwa polisi tumekuta yamejazwa kwenye kitabu cha Muhimbili, lakini polisi tulipokwenda kutoa hizo taarifa walisema hawana taarifa za mtu yeyote kupotea wala hawajua chochote kuhusu jambo hili kumbe wao ndio wamepeleka mwili polisi.

A post shared by FREEMAN MBOWE (@freemanmbowetz) on


VIDEO: POLISI KINONDONI KUHUSU MWILI WA KIONGOZI WA CHADEMA ULIOOKOTWA COCO BEACH…

Soma na hizi

Tupia Comments