Tangaza Hapa Ad

AyoTV

‘Tulipata wakati mgumu kumtambua Mzee Sitta kama bado ni kada wa CCM’ – Mbowe

on

Freeman Mbowe ni mbunge wa jimbo la Hai na mwenyekiti wa CHADEMA taifa ambaye leo November 11 2016 alipata nafasi ya kuongea wakati wa kuuaga mwili wa Spika mstaafu Samuel Sitta ndani ya bunge Dodoma.

Mzee Sitta tulimuona kama kiongozi asiekua mbaguzi wa kiitikadi, aliamini katika kubadilisha kwenda kwenye ubora katika nafasi yote ya utumishi wa UMMA aliyoihudumia, alikua mtu aliejaza matumaini watu wote aliowaongoza wakati wote, alikua mtu wa kuunganisha makundi yote‘ – Mbowe

Mara nyingine sisi wapinzani tulipata wakati mgumu sana wa kumtambua Mheshimiwa Sitta bado ni kada wa CCM sababu alikua na uwezo wa kutujaza matumaini, kutupa fursa ya kutusikiliza lakini mwishoni tunakuja kugundua bado ni wa CCM‘ – Freeman Mbowe

Kutazama yote aliyosema Freeman Mbowe tazama hii video hapa chini

VIDEO: Waziri Mwakyembe alivyoshindwa kujizuia na kumwaga machozi akimuombea Marehemu Samwel Sitta mwili wake ulipopelekwa bungeni

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement