Tangaza Hapa Ad

Mix

‘Scorpion’ anayetumiwa kumtoboa macho Said alivyopandishwa kizimbani leo

on

Kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama ‘Scorpion’ anayetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho imetajwa leo tena kwenye mahakama ya Ilala Dar es salaam.

Upande mashitaka uliiomba mahakama kuliondoa shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha linalomkabili Salumu Njwete kwa nia ya kutotaka kuendelea nalo.

Kutokana na ombi hilo hakimu Adelf Sachole alikubaliana na ombi hilo kuliondoa shitaka hilo kupitia kifungu cha 91 (1) ambapo kinampa mamlaka mkurugenzi wa mashitaka (DPP) kuondoa mashitaka muda wowote ilimradi isifike kwenye hukumu.

Baada ya saa kadhaa alifunguliwa shitaka hilohilo tena kwa hakimu mwingine Frola Haule, shtaka hilo ni la unyang’anyi kwa kutumia silaha alilolifanya September 6 2016 Buguruni sheli Dar es salaam na kuchukua vitu vyenye tahamani ya  sh 476,000, Salumu alikana mashitaka hayo.

Kutokana na kesi inayomkabili kisheria haina dhamana amerudishwa rumande na kesi hiyo itatajwa tena November 2 2016

ULIKOSA HII YA KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO BUGURUNI KUMSIMULIA RC MAKONDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement