Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Kauli ya RC Makonda kuhusu ujio wa Rais Kagame

on

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda ametoa kauli kwa Watanzania na wakazi wa DSM kuhusu ujio wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Kupitia taarifa yake, leo January 12, 2018 RC Makonda amesema kuwa Rais Kagame anatarajiwa kutembelea Tanzania January 14, 2018 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Kutokana na ujio huo, RC Makonda amewataka Watanzania na hasa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Kagame ambaye baada ya kutua Airpot Dar es Salaam ataongozana na mwenyeji wake Rais Magufuli hadi Ikulu ya Magogoni kwa ajili ya mazungumzo.

“Hakuna nchi inayoweza kwenda bila Amani, upendo na mshikamano, hivyo hakuna mgeni anayeweza kuitembelea nchi kama hakuna vitu hivyo, tunayo furaha kwa ujio wa Kagame tunamkaribisha sana,”– RC Makonda

VIDEO: KOSA ALILOLIBAINI RC MAKONDA KATIKA TUKIO LA MOTO BUGURUNI

 

Soma na hizi

Tupia Comments