PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Baada ya miaka 20, mwanamke akiri kuteka kichanga….ilikuwaje?

on

Kutoka South Carolina nchini Marekani, mwanamke mmoja amekiri mbele ya Mahakama kuwa aliiba mtoto miaka 20 iliyopita katika hospitali moja kwenye mji huo na kutoroka naye kisha kumkuza mtoto huyo hadi kuwa mkubwa.

Mwanamke huyo Gloria Williams, 52, ameeleza kuwa siku ya tukio hilo alivaa na kujifanya nesi kisha kuingia katika chumba cha hospitali ya Jacksonville, Florida ambacho mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa amelala na mtoto wake na kutekeleza tukio hilo.

Kwa upande wa mama mzazi Shanara Mobley amesema siku hiyo alipoibiwa binti yake Kamiyah Mobley, aliingia mwanamke huyo aliyekuwa amevaa nguo kama Muuguzi wa hospitali hiyo na ndipo alipomuomba amsaidie kumuweka mwanaye kwenye kitanda cha watoto lakini mwanamke huyo alimchukua mtoto huyo na kuondoka naye upesi.

Ilivyokuwa katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo

Alichozungumza Diamond Platnumz na Hamisa baada ya kutoka Mahakamani

 
 

Soma na hizi

Tupia Comments