Top Stories

Mahakama imeshindwa kutoa hukumu kesi ya Wema

on

Leo July 16,2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kutoa hukumu ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Wema Sepetu na wafanyakazi wake 2 kwa sababu kuna baadhi ya vitu havijakamilika.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mawakili wa upande wa utetezi kufunga ushahidi wao.

Baada ya Wema na washtakiwa wenzake kufika mahakamani hapo, Hakimu Simba amesema kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa hukumu lakini kuna baadhi ya vitu havijakamilika, hivyo anaahirisha hukumu hadi July 20,2018.

Mbali ya Wema, washtakiwa wenzake ni Angelina Msigwa na Matrida Abas.

Awali kabla ya kupangwa kwa tarehe ya hukumu Wema na wafanyakazi wake walijitetea, ambapo Wema amedai kuwa ni kweli nyumbani kwake kulikutwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi na vipisi.

Katika hoja zake, Wema amedai kuwa hajui vitu hivyo ni vya nani  kwa sababu yeye ni msanii wa Filamu na nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya Party na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mchana. 

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.

Alichozungumza Wema baada ya Mahakama kushindwa kutoa hukumu

BREAKING: Waziri Mbarawa atengua Mkurugenzi wa Maji

Soma na hizi

Tupia Comments