Top Stories

Msaidizi wa Trump afichua hali ilivyo katika Ikulu ya White House

on

John Kelly ambaye ni msaidizi wa karibu wa rais Donald Trump ameripotiwa kusema kwamba ikulu ya White House ni mahali duni pa kufanyia kazi akitaja mizozo ya kila mara kwenye ikulu hiyo na uvujaji wa siri kama baadhi ya changamoto ambazo ameshindwa kutatua.

Matamshi ya Kelly ambayo yalichapishwa na jarida la New York Times hapo jana ni mojawapo ya visa vya uvujaji kutoka ikulu ya White House ambavyo vinaashiria kudodora kwa mazingira ya kazi katika ikulu hiyo chini ya utawalaย wa Trump. โ€œWengi wanaofanya kazi White House wanaonyesha dalili ya kutaka kujiuzulu au kutokuwa na haja,โ€ jarida hilo lilisema.

Kelly ambaye alistaafu kama jenerali katika jeshi aliteuliwa na Trump kuwa mkuu wa utumishi wa umma mwaka jana.

Wakati wa kuteuliwa kwake Kelly alikwa na ushawishi mkubwa kwa Trump kabla ya ushawishi huo kuisha. Mapema huu mwaka Kelly aliripotiwa kuonyesha kukerwa na hali ya kazi na kutishia kujiuzulu.

Maagizo aliyotoa Naibu Waziri Kilimo Dr. Mwanjelwa katika ziara Njombe

Soma na hizi

Tupia Comments