Top Stories

Mume wa Amber Rutty alivyoanguka Mahakamani, akimbizwa Hospitali (+video)

on

January 10, 2019 Mume wa msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ ambaye ni Said Mtopali amedondoka ghafla katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu muda mfupi baada ya kesi yao kuahirishwa.

Amber Rutty na Mumewe walifikishwa Mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Kesi ya Washtakiwa hao imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando hadi February 11,2019 baada ya Wakili Neema Mbwana kusema upelelezi haujakamilika.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Washtakiwa hao walianza kuondoka katika viwanja vya Mahakama hiyo ambapo Mtopali wakati anashuka kwenye ngazi ndipo alipoanza kujisikia vibaya na ghafla kudondoka.

Kutokana na hatua hiyo watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake walianza kumpepepea ili kumpatia msaada wa kwanza lakini baadaye walimtoa katika viwanja vya Mahakama hiyo ili kumpeleka hospitali.

RC MWANRI AMVAA MHINDI KISA WAFANYAKAZI “WHERE IS MIKATABA NOW, BISHA UONE”

Soma na hizi

Tupia Comments