Top Stories

Mfanyakazi wa ndani amuua Mwajiri wake pamoja na Kichanga

on

Leo June 8, 2018 Mfanyakazi mmoja wa ndani amemuua mwajiri wake Elizabeth Achieng pamoja na kichanga chake chenye miezi mitatu huko Kisumu nchini Kenya.

Imedaiwa kuwa mfanyakazi huyo alianza kwa kumpiga mtoto mpaka akamuua kisha akamfata mama yake na kumchoma kisu mara kadhaa na kisha kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali.

Kwa sasa jeshi la Polisi Kisumu linamtafuta mfanyakazi huyo ambaye ametokomea sehemu  isiyojulikana.

Taarifa zinasema kuwa katika tukio hilo  mfanyakazi huyo hakumgusa binamu wa marehemu aliyekuwepo eneo la tukio.

Aidha inasemekana kuwa mfanyakazi huyo alikuwa anaendana kiumri na mwajiri wake  kitu kilichokuwa rahisi kwa yeye kutekeleza tukio hilo.

‘Ma-role model ni Diamond na Alikiba, Hatuwezi kuwa Taifa lenye uchumi imara’ Eng. Barozi

FULL VIDEO: Mwili wa ‘Sam wa Ukweli’ ulivyotolewa Mwananyamala kwenda kuzikwa

Soma na hizi

Tupia Comments