Top Stories

PICHA 6: Amsha amsha ya Kombe la Dunia ofisi za DSTv kumenoga

on

Leo June 14, 2018 DStv ambayo itaonyesha mechi zote za kombe la dunia 2018, imeanza shamra shamra za michuano hiyo. Siku ya leo katika ofisi za DStv kumekuwa na shamrashamra za kila aina ikiwemo ngoma, michezo mbalimbali pamoja na mashindano kwa wafanyakazi na wateja ambapo watu wamekuwa wakijinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo Tshirts, kofia, mipira na kadhalika. DStv pia itarusha matangazo hayo kwa lugha ya kiswahili.

Wakati huohuo DStv inaendelea na ofa yake kabambe ambapo kwa Sh. 79,000 tu unapata set nzima ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure!

Waigiza sanamu wakiwa wamejipanga mbele ya ofisi za MultiChoice Tanzania ikiwa ni sehemu ya amsha amsha za michuano ya kombe la Dunia la FIFA 2018. DStv itaonyesha mechi zote za kombe hilo kutoka Urusi na pia kurusha matangazo hayo kwa lugha ya Kiswahili.


Moja ya mabalozi wa DStv Riyama Ali (katikati) akiwa na maafisa waandamizi wa DStv katika shamrashamra za uzinduzi wa kombe la dunia katika ofisi za DStv leo


Baadhi ya wafanyakazi wa DStv wakishangilia wakati wa shamrashamra za uainduzi wa kombe la dunia


Waigiza sanamu wakiwa mbele ya ofisi za MultiChoice (DStv) ikiwa ni sehemu ya amsha amsha za michuano ya kombe la dunia


Meneja Biashara wa MultiChoice David Nsimba (kushoto) na Mkuu wa Uhusiano wa kampuni hiyo wakiserebuka ngoma ya Simba Theatre Troupe wakati wa shamrashamra za uzinduzi wa Kombe la Dunia 2018


Baadhi ya wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania wakiwa na fulana maalum za Kombe la Dunia 2018

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments