Top Stories

Mwili wa Mwanzilishi wa Tukuyu Stars kuchomwa moto kesho, Mwanae azungumza

on

Mwili wa aliyekuwa mwanzilishi wa klabu ya Tukuyu Stars Ramnik Patel maarufu kwa jina la Kaka unatarajiwa kuzikwa kwa kuchoma moto jumatano hii kwenye makaburi ya Sabasaba yaliyopo jijini Mbeya.

Kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ukisubiria kuwasili kwa watoto wake wawili walioko Uingereza.

Kulingana taarifa za familia watoto wake Sangita na Tanoja watawasili nchini muda wowote na kushiriki mazishi ya baba yao.

Anna Karadia ni shemeji wa marehemu Patel ameelezea kuwa kinachosubiriwa ni watoto ili washiriki kumhifadhi Patel kwenye makazi yake ya milele.

Anna Karadia shemeji wa marehemu Hinaben ni moto wa mwisho wa marehemu Patel kati ya watoto wake watatu.

Anaeleza kuwa familia yao imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na nguzo ya familia.

Hata hivyo hakusita kumwelezea marehemu babake kwa jinsi alivyomfahamu.

Hinaben Patel mtoto wa marehemu ratiba kamili ya kuuaga mwili wa Kaka ni pamoja na kuuzungusha kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ikiwa ni kuenzi kauli aliyoitoa enzi za uhai wake.

Kutana na Witness…Dereva Mwanamke wa basi la DAR-ARUSHA (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments