Top Stories

Mkurugenzi TIC atangaziwa neema na Balozi wa China, ujio wa Makampuni 26

on

Balozi wa China nchini Bi Wang Ke na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe wamefanya kikao cha kazi katika ofisi za TIC, DSM. Moja ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni ufafanuzi wa masuala kuhusu uwekezaji hapa nchini hususani kwa makampuni ya kutoka China yaliyowekeza Tanzania.

Mwambe ametoa ufafanuzi kuhusu sheria ya kutoa vivutio vya uwekezaji hasa vinavyohusu msamaha wa kodi kwa wawekezaji amesema kampuni za Kichina ziache kutumia taarifa za madalali na badala yake wafike TIC kupata taarifa mbalimbali za nchi kuhusu uwekezaji.

“Kituo hakipo hapa kumkwamisha mwekezaji, tupo kwa ajili ya kusaidia kuanzisha uwekezaji wake nchini kwa kuwa tunatambua umuhimu wa uwekezaji huo kwa nchi’ Mwambe.

Baada ya maelezo hayo Balozi ameridhishwa na amepongeza Serikali kwa kusimamia uwekezaji kwa uwazi na kufuata sheria na kwamba China inafurahia jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuboresha mazinga ya biashara na uwekezaji nchini.

“Mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa na ndiyo sababu kubwa  ya makampuni mengi ya China kuendelea kuonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania” Balozi

Vilevile Balozi amemtaarifu Mwambe kuwa December 1, 2018 msafara wa wafanyabiashara wapatao 50 unaojumuisha makampuni 26 kutoka China utafika nchini  ikiwa ni mojawapo ya mpango wao wa kutembelea nchi tatu za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda.

Lengo la ziara ya wafanyabiashara hao Afrika Mashariki ni kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta mbalimbali. Hata hivyo kwa kutambua uwepo wa mahusianao mazuri tena ya muda mrefu yaliyopo kati ya Tanzania na China msafara ulikubaliana uanzie Tanzania kabla ya kwenda nchi nyingine.

Msafara unaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Uhusiano kati ya Nchi zinazoendelea  Lyu Xinhua.  Kampuni zinazokuja nchini zipo katika Sekta za Viwanda, Ujenzi, Afya, Maji, TEHAMA, Fedha, Elimu.

Ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao wanapata taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanznaia (TPSF), Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI),Ubalozi wa China nchini na Ubalozi wa Tanznaia nchini China wanaratibu Kongamano la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na China litakalofanyika December 3,2018 Serena, Hotel Dar es salaam.

Balozi amewaomba Watanzania kutumia kongamno hilo kama chombo muhimu cha kutolea taarifa za kuhamasisha na kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China kwa kuzingatia kwamba wafanyabiashara wanaokuja ni wale wenye nia ya kuwekeza Afrika na watatembelea pia nchi nyingine kwa madhumuni ya kujionea mazingira na fursa za uwekezaji.

Hivyo matarajio ya Balozi ni kwamba Tanzania kama nchi itatumia fursa hiyo kueleza kinagaubaga fursa za uwekezaji na sababu za kuwekeza Tanzania na sio nchi nyingine.

Balozi kwa Niaba ya Serikali ya China amemuomba Mwambe kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania aendelee kutoa mwongozo stahiki kwa makampuni ya China ambayo tayari yanafanya uwekezaji wake hapa nchini  pamoja na kuwakumbusha sheria na taratibu za uwekezaji zinazotakiwa kufuatwa. Kwa kufanya hivyo,kutawezesha makampuni hayo kuwa mabalozi bora kwa makampuni mengine ya China  yenye nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

Mwambe amemhakikishia Mhe. Balozi utayari wa TIC wakati wote kupitia mfumo wake wa Huduma za Mahala Pamoja kwa Wawekezaji kuendelea kusaidia kutatua changamoto za wawekezaji wote nchini ikiwemo wale wa kutoka China Kwa takwimu za TIC kati ya 1990-May, 2017, China inashika nafasi ya kwanza kati ya mataifa kumi yanayoongoza kuwekeza Tanzania.

Mwisho, kwa wafanyabiashara wenye nia ya kushiriki kongamano kati ya Tanzania na China wanaweza kuwasiliana na Bi. Diana Ladislaus 0719 653 079 kwa maswali au Bi. Lilian Ndossi 0784323068 kwa usajili.

ZITTO KABWE AZUIWA KUMPA MKONO MBOWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments