Top Stories

BREAKING: Rais Magufuli amewasamehe Wafungwa 4,477, atuma ujumbe (+video)

on

Kwa mujibu wa Ibara ya 45 Ibara ndogo ya kwanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli ametangaza kuwasamehe Wafungwa 4,477 ambapo Wafungwa 1,076 watatoka siku ya Maadhimisho ya Uhuru yani December 9, 2018.

Akizungumza Ikulu leo JPM “Wafungwa 1,076 watatoka siku ya Maadhimisho ya Uhuru yani December 9, 2018, msamaha huu utawahusu Wafungwa Wagonjwa, Wazee kuanzia miaka sabini na zaidi, Wafungwa wakike walioingia Gerezani wakiwa Wajawazito” 

“Nimeamua Wafungwa waliotumikia robo ya adhabu zao wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la theluthi moja” -Rais Magufuli

“Msamaha hautawahusu Wafungwa wanaotumikia baadhi ya adhabu zikiwemo Kunyongwa, Kifungo cha maisha, biashara ya Dawa za kulevya, biashara za Binadamu, kukutwa na viungo vya Binadamu, Walionajisi, Waliowapa mimba Wanafunzi” -Rais Magufuli

MTAALAMU WA MABOMU ALIEKIMBIA JESHI NA KUWA MVUVI AFUNGUKA YALIYOMKUTA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments