Top Stories

Mfanyabiashara anaedaiwa kuwa Raia wa Uingereza afikishwa Mahakamani

on

Mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa, Michael Mlowe anayedaiwa kuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kuishi nchini bila kibali huku akiwa ni Raia wa Uingereze.

Kada huyo ambaye maarufu kama Mayko Namlowe (44), amesomewa mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka wa Idara ya  Uhamiaji, Novatus Mlay.

Akimsomea makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa mawili.

Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 306/2018, Mlay amedai Mlowe alikuwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali.

Inadaiwa May 31,2018 katika ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji iliyopo Wilaya ya Temeke akiwa raia  wa Uingereza alikutwa akiishi nchini akiwa hana Visa ama nyaraka yoyote inayomwezesha kufanya hivyo.

Katika shtaka lapili,  Mlay amedai kuwa mshtakiwa huyo alitoa maelezo ya uongo katika Idara ya Uhamiaji.

Mlay amedai kuwa mshtakiwa huyo,  May 31, 2018 katika ofisi hizo za Makao Makuu ya Uhamiaji akiwa raia wa Uingereza alitoa Maelezo ya uongo kuhusiana na uraia wake.

Kutoka na hatua hiyo aliweza kujipatia kitambulisho cha kitanzania namba 19741219_51108_00001_24 ambacho kina jina la Michael Juma Mlowe wakati akijua alichokifanya ni kosa.

Mshtakiwa huyo ambaye ni Mkazi wa Lugalo Kihesa mkoani  Iringa, baada ya kusomewa shtaka hilo alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mmbando alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika wenye barua na vitambulisho.

Mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili Kashindye Thabiti alikamilisha masharti hayo na kuachiwa.
Kesi imeahirishwa hadi November 11, 2018.

MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA BENKI YA CRDB KATAMBULISHWA

Soma na hizi

Tupia Comments