PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Top Stories

Zunguka vivutio vya Afrika Kusini kwa laki tano, unaambiwa bata kama lote

on

Leo Septemba 20,2018 nakusogezea good news kutoka kwa kampuni ya Maslow Shopping Travel ambapo imekuja na ofa inayomuwezesha Mtu kwenda kutazama vivutio mbalimbali vya Kitalii nchini Afrika Kusini kwa shilingi Laki Tano na Elfu Sitini tu (560,000) za Kitanzania.

Inaelezwa kuwa kwa ofa hiyo Mtu ataweza kwenda kujionea vivutio vya Kitalii kama vile Majengo marefu, Viwanja vikubwa vya soka, mitaa ya mji wa Soweto, soko maarufu la Locrate lililopo Soweto na kujionea bidhaa mbalimbali bila kusahau kuonja ladha ya vyakula vya asili.

Aidha ofa hiyo inajumuisha sehemu nzuri ya malazi ambapo Mtu atalala katika Hoteli za Maslow, shilling Elfu 79 kwa ajili ya vinywaji na chakula kwa kila siku atakayokaa, vocha ya shilling Laki moja na Elfu Hamsini na Nane kwa ajili ya kufanyia manunuzi, WI-FI na sehemu ya kupaki chombo cha moto bure.

Na Tiketi ya bure ya kwenda kutembelea kila baada ya nusu saa Sandton Gautrain, Sandton City Mall na Nelson Mandela Square.

BREAKING: KIVUKO CHA MV. NYERERE KIMEZAMA KIKIWA KIMESHEHENI ABIRIA

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments