Top Stories

Mama amkaba Mtoto wake na kumtupa Mtoni

on

Leo June 9, 2018 Polisi Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata Mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumkaba shingoni mtoto wake wa miaka 5 na kisha kumtupa katika mto Rutui.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa Mwanamke huyo mwenye miaka 23 ambaye anaishi peke yake, baada ya kutenda tukio hilo alimtupa mwanae kwenye mto na kukaa kimya akiamini kuwa maiti ya mtoto wake itachukuliwa na maji na kupelekewa sehemu isiyojulikana.

Duru za kuaminika zinasema kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo walianza kumuulizia mtoto  na mtuhumiwa akawa anawajibu  kuwa na  yeye anashangaa kutoweka kwa mwanae.

Aidha mwili wa mtoto huyo ulionekana ukielea katika mto Rutui asubuhi ya June 9 na ndipo wakazi wa eneo hilo ikiwemo mtuhumiwa waliwaita Polisi na kuutoa mwili wa mtoto huyo kisha wakamkamata mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa Polisi wa kituo cha Kirinyaga Yaya Chome amesema kuwa mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya kusudio la kutaka kuua katika mahakama ya Kerugoya.

Chanzo cha mama huyo kutenda tukio hilo la kinyama bado hakijawekwa wazi.

‘Tusikutane katika misiba, tungeweza kuchelewesha vifo vya Maria na Consolata’ Mwenyekiti Iringa

Soma na hizi

Tupia Comments