PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

IKULU: Rais Magufuli amteua Msekwa na Viongozi wengine watano leo

on

Leo December 6, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Taasisi za umma ambapo amemteua Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology – MUST).

President JPM amemteua Zakia Hamdani Meghji kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Prof. Esnati Osinde Chaggu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Pia JPM amemteua Dkt. Samwel Gwamaka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Rais Magufuli amemteua Mej. Jen. Mstaafu Michael Isamuhyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Mwingine alieteuliwa Prof. Gaspar Stephen Mhinzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).

MAAJABU TANGA MAJI YANAYOCHEMKA, USHIRIKINA WATAWALA | NG’OMBE ZACHINJWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments