Top Stories

RPC Muroto afunguka alivyomnasa Mkurugenzi akijifanya Usalama wa Taifa (+video)

on

December 7, 2018 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma RPC Gilles Muroro amekutana na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya baadhi ya matukio ya uhalifu waliyofanikiwa kuyakabili katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka ambapo miongoni mwa matukio hayo ni watuhumiwa wawili waliojifanya usalama wa taifa na kuwatapeli watu.

“Tumemkamata Salum Pwao mkazi wa DSM aliyekuwa akijifanya ni Afisa wa PSSSF akiwadanganya watu kuwa anauwezo wa kuwasaidia kupata mafao yao kwa haraka. Hivi ni vituko vya matapeli kuelekea mwisho wa mwaka nasema Dodoma tunaendelea na msako na matapeli wote wanaofikiri hapa kuna fursa basi wafahamu fursa pekee watakayoipata ni kwenda gerezani”-Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto

MTAALAMU WA MABOMU ALIEKIMBIA JESHI NA KUWA MVUVI AFUNGUKA YALIYOMKUTA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments