Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Sahau kuhusu kijani kibichi kichwani, hii ni mpya tena ya Ben Pol

on

Mkali wa RnB Ben Pol amezua gumzo tena kwenye mitandao ya kijamii kutokana na vazi lake alilolivaa kwenye utambulisho wa ngoma yake mpya ya “Zai” aliyoitambulisha rasmi leo May 15,2018 Clouds Fm katika kipindi cha XXL.

Ben Pol ni staa ambaye amezoeleka na mashabiki kuvaa nguo za kawaida na wengi kudai kuwa hana muonekano wa kistaa kutokana na mavazi anayoyavaa, shati lake lililochanika aliloenda nalo XXL limewapa mashabiki maswali mengi na kujiuliza kuhusu muonekana huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ben Pol kuchukua headlines kutokana na muonekano wake, mara ya kwanza alichukua headlines kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka rangi ya kijani kwenye nywele zake kitu ambacho kiliacha maswali mengi lakini baada ya muda aliamua kutoa.

Vitu anavyoruhusiwa na asivyoruhusiwa Lulu kufanya kipindi hiki akitumikia kifungo cha nje

Soma na hizi

Tupia Comments