Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Hawa ndio washindi wa Tuzo za Vijana 50 wa Kitanzania wenye Ushawishi

on

Tuzo za Vijana 50 wa Kitanzania wenye Ushawishi (50 Tanzania Most Infuential Young Tanzanians) zilizoandaliwa na Avance Media zimetangaza washindi wake leo January 16, 2018 ambapo Mtu wako wa Nguvu, Mr Countdown Millard Ayo amekuwa mshindi kwenye kitengo cha Vyombo vya Habari.

Washindi wengine ni pamoja na Mwanasoka Mbwana Samatta kwenye category ya Michezo, mwingine ni Wakili Peter Kibatala kwenye category ya Sheria na Uongozi, Yusuph Bakhresa akichukua tuzo kwenye category ya Biashara.

Wengine ni Mwanamuziki Alikiba ambaye amechukua tuzo ya Burudani, Faraja Nyalandu akichukua category ya Biashara za Kijamii na Asasi za Kiraia, Mitindo ya Maisha tuzo yake imechukuliwa na Jackline N. Mengi na tuzo ya Sayansi na Teknolojia imechukuliwa na Jumanne Mtambalike.

Mbwana Samatta pia amekuwa Mshindi wa Jumla (Overall Winner) kwa kupata kura nyingi zaidi kuzidi wote walioshindania tuzo hizo akifuatiwa na Wakili Kibatala na Millard Ayo.

Baada ya Lowassa kusema alichoongea IKULU, Rungwe ameongea

Je kuna msako wadada wanaovaa nguo fupi DSM?

 

 

Soma na hizi