Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kitu Faraja Nyalandu ameandika baada ya kuona Miss TZ 2016 anaandamwa

on

Baada ya shindano la Miss Tanzania 2016 kufikia kileleni October 29 2016 Mwanza na mshindi kupatikana, yalizuka maneno juu ya mshindi Diana Edward Loy yanayohusu umri na elimu yake.

Leo October 31 2016 aliyekua Miss Tanzania 2004 Faraja Kotta Nyalandu ametumia ukurasa wake wa Intagram kumuandikia ujumbe wa kumtia moyo na kukumbushia ilivyokua kwake baada ya kutangazwa mshindi mwaka 2004.

screen-shot-2016-10-31-at-3-47-46-pm

Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda, asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano. nilipigiwa simu kuamshwa, nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani. Nilitetemeka

Nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili, nilijuta kushiriki Miss Tanzania… nilikua mdogo na sina uelewa wa mambo mengi, ndio nilikua nimefikisha umri wa miaka 19, na hapo tu ndio natoka shule ya boarding tena ya Katoliki’ sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua’ – Faraja Nyalandu

screen-shot-2016-10-31-at-3-47-11-pm

Iliwibidi wazazi wangu ambao wameshafariki (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri, haikua rahisi… nilijifunza na leo hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji… nilijifunza kupitia mabaya na nashukuru kwa fundisho hilo’ – Faraja

Kwa kumalizia Faraja ameandika ‘Namshukuru Mungu nilijifunza mapema, kuna sehemu ya nguvu niliyonayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja, usijitafutie laana za rejareja… sasa kwa Miss Tanzania mpya uliyechaguliwa, fanya yako… wengine tuliobaki tujenge zaidi ya kubomoa. upendo haugharimu chochote

Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda. Asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano. Nilipigiwa simu kuamshwa. Nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani. Nilitetemeka, nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki Miss Tanzania. I was young and naive. I had just turned 19, coming straight from the safety nets of Catholic nuns boarding schools. Sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua. It took my parents (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri. I had to dig deep inside me to regain my purpose. I was exposed to a cruel world and yes, I quickly learnt, it is what it is. Leo hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji. I learnt the hard way but I am grateful for the lesson. Thank God I learnt early. Kuna sehemu ya nguvu niliyo nayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona. Lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja. Usijitafutie laana za reja reja. To the newly crowned Miss Tanzania, Do you honey! To the rest of us, tujenge zaidi ya kubomoa. Love doesn’t cost a thing! God bless, Faraja

A photo posted by Faraja Nyalandu (@farajanyalandu) on

MWANZO MWISHO: Tazama fainali ya shindano la Miss Tanzania 2016 lilivyofanyika Mwanza, bonyeza play kwenye hii video hapa chini….

ULIIKOSA? Alichosema mshindi wa tatu wa Miss Tanzania kuhusu ushindi wa Miss Tanzania 2016? bonyeza play hapa chini kumtazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement