Top Stories

Mwanaume aishtaki hospitali kwa kutumia sehemu zake za siri….Ilikuwaje?

on

Leo June 11, 2018 Mwanaume mmoja nchini Kenya ameishtaki hospitali ya Agha Khan kwa kutumia nyeti zake kuwafundishia wanafunzi wa kike wanaosoma udaktari kinyume na matakwa yake.

Mwanaume huyo ambaye alipenda kutambulika kama DK kwa ajili ya kutunza faragha yake ,amesema kuwa alienda katika hospitali hiyo kama mgonjwa kumuona Dokta Samnakay na sio kutumika kama sampuli ya kufundishia.

Dk amesema kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye sehemu zake za siri hivyo ikambidi aende katika hospitali hiyo ili kupatiwa matibabu.

“Wakati nimelala katika  chumba cha kufanyiwa vipimo huku nikiwa mtupu waliingia Wasichana wawili ambao waliniambia kuwa wao kiumri ni wadogo sana kwangu kitu kilichonifanya nishituke sana” amesema DK

Aidha Dk anasema kuwa wakati akichukuliwa vipimo, Daktari aliwauliza maswali Wanafunzi hao wawili kitu kilichomfanya agundue kuwa amegeuzwa sampuli ya kufundishia bila yeye kujua.

Kwa sasa Dk ameifungulia mashtaka hospitali hiyo akidai afidiwe baada ya kugeuzwa sampuli ya kufundishia bila ridhaa yake huku hospitali hiyo ikitakiwa na mahakama kuleta utetezi wake Julai 18.

LIVE MAGAZETI: Tundu lissu: hatusalimiki, Samia, Askofu Shoo wafunguka mazito

Soma na hizi

Tupia Comments